Home BUSINESS BENKI YA AKIBA YATOA ELIMU YA FEDHA KWA WADAU MBALIMBALI

BENKI YA AKIBA YATOA ELIMU YA FEDHA KWA WADAU MBALIMBALI

 

Na: Mwandishi wetu

Benki ya Akiba imesema itaendelea kuunga mkono serikali kwa kutoa elimu ya fedha huku ikiboresha huduma zake nchi nzima ili kusaidia kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuchochea kukua kwa uchumi wa Taifa.

Ameyasema hayo Juni 14 ,2024 Jijini Dodoma Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Akiba Bw Silvest Arumasi wakati wa kuhitimisha mafunzo ya elimu ya fedha yaliyojumuisha viongozi wa benki hiyo ,watumishi kutoka Wizara , taasisi na ofisi mbalimbali za serikali lengo likiwa ni kubadilishana ujuzi na kujenga mahusiano mazuri huku wakifahamiana na kuweka mikakati ya pamoja namna ya kuwahudumia watumishi wa Umma kwa weledi zaidi na kujibu maswali na kujibu maswali huku wakitatua kero zinazojitokeza kiutendaji

Mkurugenzi Arumasi amebainisha kuwa benki hiyo itawaangalia wananchi wa Dodoma kwa upekee kutokana na fursa mpya zilizopo katika Jiji hilo kwani serikali imekuwa ikiendeleza na kustawisha Makao makuu ya Nchi hivyo ametoa rai kwa wananchi kujishughulisha na biashara na wanapokwama benki hiyo ipo kutoa mikopo kwa riba nafuu .

“Tunaahidi kuwa benki itaendelea kuunga mkono serikali kwa kuwasadia wananchi kuwapatia mikopo nafuuu ili kuinua mitaji yao pia kupanua wigo wa huduma nchi nzima ili kufikia azma ya kutoa mchango mkubwa wa kuwepo kwa huduma shirikishi za kifedha yaani financial inclusion” amesema Mkurugenzi Arumasi

Naye Bi Upendo Makula, Meneja wa Tawi la ACB – Dodoma aliwashukuru sana washiriki wote kwa kuitikia mwito kwa ujumla wao

Aidha washiriki wote waliishukuru Benki ya Akiba kwa mada nzuri za semina hiyo na wameahidi kutumia elimu hiyo kama chachu katika utendaji wao wa kila siku kwani wamejengewa msingi imara wa uelewa wa maswala ya fedha

Previous articleMAJALIWA: WATANZANIA TUENDELEE KUDUMISHA AMANI, UPENDO NA MSHIKAMANO
Next articleUMMY MWALIMU ANAVYOWAWEKEA WANAWAKE WA JIJI LA TANGA MAZINGIRA WEZESHI KUWAINUA KIUCHUMI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here