Home BUSINESS Dkt. NGENYA: SERIKALI IMEKUWA IKITENGA ZAIDI YA MILIONI 250 KUHUDUMIA WAJASIRIAMALI WADOGO

Dkt. NGENYA: SERIKALI IMEKUWA IKITENGA ZAIDI YA MILIONI 250 KUHUDUMIA WAJASIRIAMALI WADOGO

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Athuman Ngenya akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Mafanikio na Majukumu ya Shirika hilo katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kwenye mkutano na Wahariri na waandishi wa Habari, kilichofanyika leo Aprili 15,2024, Jijini Dar es Salaam, chini ya Uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Afisa Habari Mwandamizi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina, Sabatho Kosuri, akizungumza alipokuwa akitoa neno la utangulizi katika mkutano huo.

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM 

Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia Shirika la Viwango Tanzania (TBS), imekuwa ikitenga fedha zaidi ya milioni 250 kwaajili ya kuhudumia wajasiriamali wadogo.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hilo, Dkt. Athuman Ngenya, alipokuwa akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Mafanikio na Majukumu ya taasisi hiyo katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kwenye mkutano wa Wahariri na waandishi wa Habari kuliofanyika leo Aprili 15,2024, Jijini Dar es Salaam, chini ya Uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Amesema kuwa uamuzi huo wa Mheshimwa Rais, umelenga kuwainua wajasiriamali na wafanyabiasha wadogo kufikia malengo yao, kukidhi vigezo vya ubora wa bidhaa zao na hatimaye kuuza kwenye masoko ya ndani na nje ya nchi.

“Katika kipindi cha miaka mitatu, jumla ya leseni za ubora wa bidhaa 2,106 zilitolewa kwa wazalishaji mbalimbali wa bidhaa hapa nchini, sawa na asilimia105.3 ya lengo la kutoa leseni 2,000” amesema Dkt. Ngenya.

Aidha amefafanua kuwa kati ya leseni hizo, jumla ya leseni 1,051 zilitolewa bure kwa Wajasiriamali wadogo 21, ambapo jumla ya Wazalishaji na Wajasiriamali 5,789 wamenufaika kwa kupatiwa mafunzo Kwa kipindi cha miaka mitatu.

“TBS imeendelea kutoa mafunzo kwa wajasiriamali wadogo (MSEs) na wazalishaji ili kuwawezesha kuzalisha bidhaa zinazokidhi matakwa ya viwango vya ubora na usalama na hatimaye kukidhi ushindani wa masoko ya ndani, kikanda na kimataifa” amefafanua.

Ameongeza kuwa katika kipindi cha miaka mitatu Shirika hilo liliandaa jumla ya viwango1,721 vya kitaifa sawa na asilimia 101.2. ya lengo la kuandaa viwango 1,700 vilivyoandaliwa katika nyanja mbalimbali.

“TBS imeshiriki katika uandaaji wa viwango vya kibiashara vya Afrika Mashariki na Afrika nzima, Kuweka mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara na wazalishaji, utoaji wa leseni za Alama ya Ubora.

“Ikumbukwe kwamba tuna makubaliano katika nchi za Afrika mashashiriki na Afrika kwa bidhaa zenye nembo ya ubora kuingia na kuweza kuuzwa katika nchi hizo” ameongeza Dkt. Ngenya

Previous articleSERIKALI YATOA ZAIDI YA MILIONI 216 HUDUMA ZA  AFYA WAATHRIKA WA MAFURIKO 
Next articleCCM TUSIBWETEKE, UCHAGUZI HUU UNA USHINDANI MKUBWA-KINANA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here