Home LOCAL SILAA AKABIDHI MAGARI YENYE THAMANI YA BIL.2.7 MRADI WA UBORESHAJI MILKI ZA...

SILAA AKABIDHI MAGARI YENYE THAMANI YA BIL.2.7 MRADI WA UBORESHAJI MILKI ZA ARDHI NCHINI

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa mapema leo amekabidhi magari 16 yenye thamani takriban Bil. 2.7 za Tanzania zitakazotumiwa na Mradi wa Usalama wa Uboreshaji wa Milki za Ardhi Nchini ambazo ni sehemu ya magari mengine kama hayo 54 yatayowasilishwa baadae ikiwa ni hatua muhimu ya utekelezaji wa mradi huo.

Akiongea na vyombo vya habari mara baada ya makabidhiano hayo Waziri Silaa ameweka wazi kuhusu matumizi sahii ya magari hayo ikiwemo kuyatunza na kuyafanyia matengenezo kwa wakati ili utekelezaji wa mradi huo uweze kutekelezeka kama ilivyopangwa.

’Waziri Silaa ameonya watumiaji wa magari hiyo kuzingatia weledi wa kazi yao na kuyatumia kama inavyotakiwa akiongeza kuwa magari hayo yasuije yakatumika kufanya mambo mengine ikiwemo kubeba mikaa au kushiriki katika shughuli za kijamii ikiwemo harusi.

‘’Magari haya yatumike kwa kazi za mradi wale wote watakao kabidhiwa magari haya wayatumie vizuri, wayatunze tusione magari haya yamebeba mkaa au kufanyika katika shughuli za harusi tungependa kuyaona yakifanya kazi ya Mradi tunaamini magari haya yanaenda kuongeza kasi na chachu ya utekelezaji wa mradi’’. Waziri silaa aliongeza.

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Eng. Anthony Sanga wakati akimkaribisha Waziri huyo kukabidhi magari hayo amesema thamani ya gari moja ni takribani Mil. 129.9 za Tanzania na magari hayo ni sehemu ya magari 70 yatakayonunuliwa kwa msaada wa Benki ya Dunia.

Eng. Anthony Sanga amesema mradi huo mkubwa wa Benki ya Dunia thamani ya Bil. ni 300 na utakelezaji wake unaendelea katika Halmashauri mbalimbali hapa Nchini hivyo matumizi ya magari hayo yatapelekwa katika baadhi ya Halmashauri ili kuendeleza shughuli za mradi huo.

Kwa Upande wa Mratibu wa Mradi huo Bw. Joseph I.Shewiyo amesema uwepo wa magari hayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa utekezaji wa mradi ambao umegawanyika katika sehemu kuu nnne ambazo ni Usalama wa Milki, uimarishaji mifumo ya taarifa za Ardhi na ujenzi wa miundombinu ya Ardhi.

Hafla hiyo fupi ya uzinduzi wa magari ya mradi wa uboreshaji wa usalama wa milki za ardhi yamefanyika makao makuu ya ofisi za Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi Mtumba jijini Dodoma na kushuhudiwa na viongozi na watumishi mbalilimbali wa Wizara.

 
WAZIRI  wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Jerry Silaa  akikata utepe kukabidhi magari 16 kwa aijili ya Mradi wa Uboreshaji wa Miliki za ardhi (LTIP) hafla iliyofanyika leo Februari 19,2024  mji wa kiserikali Mtumba jijini Dodoma.
WAZIRI  wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Jerry Silaa akiwasha gari kuashiria kuanza kwa matumizi ya gari mpya kwa aijili ya Mradi wa Uboreshaji wa Miliki za ardhi (LTIP) hafla iliyofanyika leo Februari 19,2024  mji wa kiserikali Mtumba jijini Dodoma.
 
WAZIRI  wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Jerry Silaa ,akimkabidhi ufunguo wa gari Katibu Mkuu Wizara  wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi. Anthony Sanga kwa ajili ya kumkabidhi  Mratibu wa Mradi huo.
 Katibu Mkuu Wizara  wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga akikabidhi ufunguo wa gari Mratibu wa Mradi huo Bw. Joseph Shewiyo  kama ishara ya kuanza kutumika kwa magari hayo kwenye Mradi wa Uboreshaji wa Miliki za ardhi (LTIP) hafla iliyofanyika leo Februari 19,2024  mji wa kiserikali Mtumba jijini Dodoma.
WAZIRI  wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Jerry Silaa,akizungumza mara baada ya kukabidhi  magari 16 kwa aijili ya Mradi wa Uboreshaji wa Miliki za ardhi (LTIP) hafla iliyofanyika leo Februari 19,2024  mji wa kiserikali Mtumba jijini Dodoma.
KATIBU  Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga,akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi  magari 16 kwa aijili ya Mradi wa Uboreshaji wa Miliki za ardhi (LTIP) hafla iliyofanyika leo Februari 19,2024  mji wa kiserikali Mtumba jijini Dodoma.
 
Mratibu  Mradi wa Uboreshaji wa Miliki za ardhi (LTIP) Bw. Joseph I.Shewiyo ,akielezea jinsi magari yatakavyotumika wakati wa hafla ya kukabidhi  magari 16 kwa aijili ya Mradi wa Uboreshaji wa Miliki za ardhi
  hafla iliyofanyika leo Februari 19,2024  mji wa kiserikali Mtumba jijini Dodoma.
 
MUONEKANO wa Magari 16 yaliyokabidhiwa na Waziri  wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Jerry Silaa kwa aijili ya Mradi wa Uboreshaji wa Miliki za ardhi (LTIP) hafla iliyofanyika leo Februari 19,2024  mji wa kiserikali Mt
Previous articleDkt. NCHIMBI ATUA KAGERA, MAZISHI YA BALOZI DK. DIODORUS KAMALA
Next articleWAZIRI KAIRUKI AZINDUA VITENDEA KAZI VYA DORIA MISITUNI VYENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 6
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here