Home BUSINESS WAZIRI MAVUNDE APONGEZA UTENDAJI CHUO CHA BANDARI

WAZIRI MAVUNDE APONGEZA UTENDAJI CHUO CHA BANDARI

Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde (kulia), akipata maelezo kuhusu masuala mbalimbali ya udahili kwa wananfunzi wanaotaka kujiunga na chuo Cha Bandari, kutoka kwa Afisa Udahili wa chuo hicho Upendo Mtinangi (wa pili kulia), wakati alipotembelea katika banda la TPA kwenye maonesho ya teknolojia ya Madini yanayoendelea katika viwanja vya EPZ Bombambili Mkoani Geita, (wa kwanza kushoto) ni Mkufunzi wa Mitambo Chuo cha Bandari. Francis Mgaya, na (wa tatu kushoto), ni Afisa Utekelezaji, Bandari ya Magarini, Bukoba, ramadhan Msuya.

Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde (kulia) akitoa pongezi kwa watumishi wa Chuo cha Bandari , huku wakipiga makofi kuashiria kupokea pongezi hizo, wakati waziri huyo alipokuwa akizungumza alipokuwa kwenye Banda la TPA katika ziara yake ya kukagua Mabanda ya washiriki katika Maonesho ya Madini Mkoani Geita.

(PICHA ZOTE NA HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo, GEITA

Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), imepiga kambi katika maonesho ya sita ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya EPZ Bombambili Mkoani Geita kutoa elimu kwa wananchi kufahamu namna ambavyo Mamlaka hiyo inavyotekeleza kwa majukumu yake kwa mujibu wa sheria.

Pamoja na mambo mengine, TPA imeshiriki katika Maonesho hayo wakiwa na Chuo chao ambacho kimekuwa kikivutia wananchi wengi kutaka kufahamu fursa za kitaaluma zitolewazo na Chuo hicho.

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde (Mb), ni miongoni mwa wageni waliotembelea katika Banda la TPA na kuonesha kuvutiwa na kazi zinazofanywa na Chuo cha Bandari Tanzania, ambapo licha ya kuwapongeza kwa kazi kubwa na nzuri wanayofanya, ametoa mwito kwa wananchi kutembelea katika Banda hilo. 

Akizungumza kuhusiana na chuo hicho, Afisa Udahili wa chuo cha Bandari Tanzania, hicho Pendo Mtinangi, amesema kuwa wameshiriki kwenye Maonesho hayo kutoa elimu kwa wananchi  kuhusu huduma za Bandari, na kwamba kuna uhusiano mkubwa kati ya huduma zao na sekta ya Madini.

“Kuna Mafunzo ya Kozi mbalimbali tunayotoa katika Chuo chetu, ikiwemo mafunzo ya uendeshaji wa mitambo ambayo baadhi yake inatumika katika sekta ya Madini,  Ujenzi na Viwanda” amesema Pendo

Chuo kinatoa mafunzo kwa ngazi za Astashahada na Stashahada, ambapo sifa za msingi ni kuanzia ufaulu wa alama D 4, za kidato cha nne.

Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde (kulia), akipata maelezo kuhusu namna mizigo mbalimbali  inavyoshushwa kwenye meli kutoka kwa Afisa Utekelezaji Bandari ya Mwanza Mussa Mange  (kushoto), wakati alipotembele katika banda hilo.

Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde (kushoto), akipokea zawadi kutoka kwa Afisa Udahili kutoka Chuo cha Mamlaka ya Bandari Tanzania  Upendo Mtinangi wakati alipotembelea kwenye  Banda la Mamlaka hiyo, katika maonesho ya teknolojia ya Madini yanayofanyika viwanja vya EPZ Bombambili Geita. (kulia),ni Afisa Utekelezaji, Bandari ya Magarini, Bukoba, ramadhan Msuya.

Baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), wakiwa katika picha ya pamoja.

Previous articleUGANDA WAJIFUNZA TEKNOLOJIA MADINI
Next articleATAKAYEKWAMISHA WAFANYABIASHARA NI ADUI NAMBA MOJA WA SERIKALI – Dkt. HASHIL
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here