Home LOCAL MAHAKAMA KUU ZANZIBAR YATUPILIA MBALI RUFAA YA JINAI

MAHAKAMA KUU ZANZIBAR YATUPILIA MBALI RUFAA YA JINAI

Na: Halfan Abdulkadir, Zanzibar.

Mahakama Kuu Zanzibar leo Jumatatu Septemba 18, 2023 imetupilia mbali Rufaa ya jinai Namba 105/2022 baina ya Suleiman Salum Mohd (40) Mkaazi wa Miembe Saba Unguja na Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar DPP.

Awali Mshtakiwa huyo alishtakiwa Kwa kosa la kumtorosha Mtoto wa Kike (08) kinyume na kifungu Namba 113(1)(a) na kosa la kumuingilia kinyume na Maumbile mtoto huyo ambapo ni kinyume na kifungu 133(a) vya Sheria Namba 6/2018.

Akisoma hukumu hiyo ya Rufaa Jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar Aziza Suwedi amesema, Mahakama ya Mkoa Vuga ilizingatia ushahidi uliotolewa Mahakamani hapo ambao haukuwa na chembe ya shaka ndani yake na ulimtia hatiani Mshtakiwa huyo .

Mahakama Kuu Zanzibar umeamuru Mshtakiwa huyo kutumikia kifungo Cha miaka 25 Jela kama ilivyotolewa na Mahakama ya Vuga mbele Hakimu Ali Simai .

Previous articleMAKAMU WA RAIS AKISHIRIKI UFUNGUZI WA MKUTANO WA SDGs – NEW YORK
Next articleRAIS DKT. SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BARABARA YA NANGANGA- RUANGWA-NACHINGWEA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here