Home LOCAL BARABARA YA RUANGWA – NANGAGA FURSA KWA WANANCHI  

BARABARA YA RUANGWA – NANGAGA FURSA KWA WANANCHI  

Na: Immaculate Makilika – MAELEZO

Wananchi wa eneo la Nandagala lililopo Wilaya ya Ruangwa Mkoa wa Lindi wamepongeza hatua ya Serikali ya kujenga barabara ya Ruangwa hadi Nangaga yenye urefu wa km 53.5 inayolenga kusaidia katika usafiri na usafirishaji wa bidhaa na mizigo kwenda maeneo mbalimbali nje ya mkoa huo.

Bi. Sofia Juma amesema kuwa kabla ya ujenzi wa barabara hiyo hali ilikuwa mbaya na kusafiri kwenda Mtwara au Dar es salaam iliwalazimu kutumia muda mwingi zaidi.

” Kwa sasa barabara hii inaendelea kujengwa na tunapongeza kwa hatua hii iliyofikia sasa hivi kwenda Dar es salaam hatutumii muda mwingi kama mwanzo”, amesema Bi Sofia.

Vilevile, Bi. Fatma Abdallah ameeleza kuwa awali kutumia barabara hiyo hasa wakati wa mvua ilikuwa shida zaidi na magari yaliharibikia njiani.

“Hata nauli imekua nafuu, kutoka shilingi 4500 hadi sasa shilingi 3000. Pia, kusafirisha mazao mfano korosho, ufuta na mbaazi imekua rahisi”, ameeleza Fatma.

Ametaja manufaa mengi ya barabara hiyo “Hata mimi binafsi nimepata ajira ya kupika chakula kwa wahandisi wanaojenga hapa na kwa kweli napata fedha za kuhudumia familia yangu”.

Aidha, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, ameweka jiwe la msingi katika barabara hiyo ya Ruangwa – Nangaga ambayo ni kati ya miradi anayotembelea mkoani humo.

Previous articleTIRA YAENDELEA VIZURI NA USIMAMIZI WA SHUGHULI ZA BIMA
Next articleRUANGWA WAJIVUNIA RAIS DKT. SAMIA 
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here