Home BUSINESS WABUNIFU SEKTA YA KILIMO WASAIDIWE- DKT MPANGO

WABUNIFU SEKTA YA KILIMO WASAIDIWE- DKT MPANGO

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango amezitaka Wizara na Taasisi husika kuhakikisha kuwa wabunifu katika sekta ya kilimo wanatambuliwa na kulindwa kisheria ili waweze kunufaika.

Mhe. Mpango ametoa agizo hilo leo tarehe 1 Agosti, 2023 alipokuwa akifungua Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima (Nanenane) yanayofanyika katika Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Mhe. Mpango amesema yanapofanyika maonesho haya ni muhimu kuwatambua wabunifu katika sekta ya kilimo, mifugo na Uvuvi ikiwa ni njia mojawapo ya kuwahamasisha na kuwasaidia kulinda ubunifu wao kisheria.

“Nimefurahi kumuona mbunifu ambaye ameunda gari inayopukuchua mahindi na bidhaa zingine, mbunifu kama huyu anapaswa kusaidiwa ili anufaike na ubunifu wake”, amesema Mhe. Mpango.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonesho hayo Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe amesema umefika wakati sasa kwa bidhaa zote za chakula na mbegu kutoka Tanzania kwenda nje ya nchi zitambulike kwa kuhusisha masuala ya Miliki Ubunifu tofauti na ilivyo sasa.

Amesema Tanzania ina utajiri wa mazao mengi ya chakula pamoja na mbegu bora zilizofanyiwa utafiti na vituo vya Utafiti vilivyopo nchini lakini vinaposafirishwa nje ya nchi havitambuliki kama asili yake ni Tanzania hivyo suala la miliki ubunifu ni muhimu kukulizingatia.

Wakala wa Usajili wa Biasahara na Leseni (BRELA) ambayo inashiriki katika maonesho hayo, mbali na kuhamasisha urasimishaji wa biashara pia itatumia fursa ya maonesho hayo kuwatembelea wabunifu mbalimbali ili kuwapatia elimu kuhusu usajili wa Vumbuzi zao BRELA ili waweze kulindwa kisheria.

Katika maonesho hayo yatakayohitimishwa tarehe 8 Agosti, 2023, yenye kauli mbiu ‘Vijana na wanawake ni Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula’, BRELA inatoa huduma za papo kwa papo za sajili na elimu kwa wadau wanaotembelea mabanda yake.

Previous articleYASEMAVYO MAGAZETI YA LEO AGOSTI 2-2023
Next articlePSSSF YAWAKARIBISHA WANACHAMA NA WANANCHI MAONESHO YA NANENANE MBEYA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here