Home LOCAL MSD YAWAPIGA MSASA WATUMISHI KADA YA UDEREVA

MSD YAWAPIGA MSASA WATUMISHI KADA YA UDEREVA

Watumishi wa MSD wa kada ya Udereva, wamejengewa uwezo kupitia mafunzo mbalimbali yanayoandaliwa na taasisi hasa katika eneo la huduma kwa wateja wakati wa usambazaji bidhaa za afya.

Mafunzo hayo yanayofanyika mkoani Morogoro yamekutanisha madereva wote wa MSD kutoka Makao Makuu na Kanda.

Mkufunzi wa mafunzo hayo Kaimu Meneja wa Rasilimali watu Ndugu. Adolar Duwe, ameeleza kuwa mafunzo hayo yana umuhimu mkubwa kwa Wataalamu wa usambazaji bidhaa za afya kwani yatawawezesha kuongeza uelewa juu ya huduma kwa wateja na namna ya kuhudumia wateja wa MSD.

Akizumgumza kwa niaba ya Maderava wa MSD Bw. Erick Kaaya, amesema mafunzo hayo yamewaongezea ujuzi, kujiamini na uelewa wa masuala mbalimbali ya muhimu katika kuhudumia wateja. Aidha ameiomba Menejimenti ya MSD, kuratibu mafunzo hayo mara kwa mara, ili kuwajengea uwezo na kuongeza tija katika utekelezaji wa shughuli za taasisi.

Previous articleYASEMAVYO MAGAZETI YA LEO IJUMAA JUNI 30 – 2023
Next articleWAFANYABIASHARA KUTOKA AFRIKA KUSINI WATEMBELEA SIDO MAONESHO YA SABASABA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here