Home BUSINESS COSTECH YAFADHIRI MIRADI 47 YA UTAFITI KUKUZA KAZI ZA WABUNIFU WA KISAYANSI.

COSTECH YAFADHIRI MIRADI 47 YA UTAFITI KUKUZA KAZI ZA WABUNIFU WA KISAYANSI.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nundu akizungumza wakati akifungua kikao kazi leo tarehe 14/6/2023 katika  Kongamano 8 la Kitaifa la Sayansi Teknolojia na Ubunifu linalofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa Cha Mikutano Cha Kumbukumbu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam (PICHA NA JOHN BUKUKU)

Baadhi ya watoa mada wakiwa katika kikoa kazi leo tarehe 14/6/2023 katika  Kongamano 8 la Kitaifa la Sayansi Teknolojia na Ubunifu linalofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa Cha Mikutano Cha Kumbukumbu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

Baadhi washiriki wakiwa katika kikao kazi  leo tarehe 14/6/2023 katika  Kongamano 8 la Kitaifa la Sayansi Teknolojia na Ubunifu linalofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa Cha Mikutano Cha Kumbukumbu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

NA: NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imefadhili miradi 47 ya utafiti yenye thamani zaidi ya Shilingi bilioni 5 jambo ambalo limesaidia kwa asilimia kubwa kuwezesha kazi zao.

Akizungumza leo tarehe 14/6/2023 Jijini Dar es Salaam wakati akifungua kikao kazi katika Kongamano 8 la Kitaifa la Sayansi Teknolojia na Ubunifu, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nundu, amesema kuwa pia katika kipindi cha miaka mitano wamefanikiwa kufadhili miradi 11 ya miundombinu ya utafiti yenye thamani zaidi shilingi bilioni 5.

Dkt. Nundu amesema kuwa ufadhili huo umewasaidia wabunifu kuanzisha makampuni kutokana na ubunifu wao katika kuboresha bidhaa na huduma wanazotoa.

“Tumeandaa muongozo ili kuhakikisha wabunifu wanafanikiwa na kusonga mbele pamoja na kutoa fedha kuwasaidia wabunifu” amesema Dkt. Nundu.

Dkt. Nundu amesema kuwa kupitia Kongamano hilo washiriki wanapaswa kujitoa katika kuchangia maoni yao kwani ni muhimu katika kuandaa ripoti ambayo inakwenda kufanyiwa kazi katika dira ya mpango wa Taifa ya  mwaka 2025 katika upande wa teknolojia na ubunifu.

Amesema kuwa serikali imeaandaa dira ya mwaka 2025 ambapo wabunifu na watafiti wanatakiwa kuchangia kuchangamkia fursa ya kutoa mawazo ili ripoti imebena maono ambayo yanakwenda kuboresha na kutengeneza dira ya Taifa.

“Lengo la Kongamano ni kuwaweka pamoja watafiti, wabunifu, wanazuoni ili waweze kuchangia mawazo yao katika kuhakikisha tunapiga hatua katika nyanja mbalimbali za maendeleo” amesema Dkt. Nundu.

Amesema kuwa katika kongamano hilo nchi mbalimbali zimeshiriki ikiwemo Afrika Kusini, Kenya, Nambia pamoja Afrika Mashariki.

Kongamano 8 la Kitaifa la Sayansi Tenknolojia na Ubunifu linalofanyika kwa siku tatu kuanzia Juni 14- 16, 2023 jijini Dar es Salaam linakwenda pamoja na uwasilishaji wa mada za ubunifu na utafiti.

Kongamano limeandaliwa na COSTECH kupitia mradi wa elimu ya juu kwa mageuzi ya Kiuchumi (Higher Education for Economic Transformation [HEET] Project) unaofadhiliwa na Benki ya Duniani.

Previous articleRAIS DKT. SAMIA AKISALIMIANA NA WANANCHI WA BUHONGWA MWANZA
Next articleRAIS SAMIA AHUTUBIA MKUTANO WA EITI KWA NJIA YA MTANDAO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here