Home BUSINESS SERIKALI, BENKI YA DUNIA KUSHIRIKIANA KUWAWEZESHA WANAWAKE KATIKA NYANJA ZOTE

SERIKALI, BENKI YA DUNIA KUSHIRIKIANA KUWAWEZESHA WANAWAKE KATIKA NYANJA ZOTE

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. John Jingu akizungumza wakati wa Kikao Kazi cha kujadili uwezeshaji kwa Wanawake nchini kilichoratibiwa na Benki ya Dunia sambamba na uzinduzi wa wa Ripoti ya Masuala ya Wanawake, Biashara na Sheria katika hafla iliyofanyika leo Machi 22, 2023 Jijini Dar es Salaam.

Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt. Nandera Mhando (katikati) akiwa na wadau wengine kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake, pamoja na Benki ya Dunia machapisho katika uzinguzi rasmi wa Ripoti ya Masuala ya Wanawake, Biashara na Sheria katika hafla iliyofanyika leo Machi 22, 2023 Jijini Dar es Salaam.

Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt. Nandera Mhando akizungumza alipokuwa akitoa hotuba yake muda mfupi kabla ya uzinguzi rasmi wa Ripoti ya Masuala ya Wanawake, Biashara na Sheria, uliofanyika leo Dar es Salaam.

Mtaalam wa Masuala ya Wanawake, Biashara na Sheria kutoka Benki ya Dunia, Daniela Behr akizungumza katika hafla hiyo.

Afisa Programu kutoka Shirika la International Finance Cooperation (IFC) akitoa mada katika hafla hiyo, iliyofanyika leo Machi 22, 2023 Jijini Dar es Salaam.

Picha mbalimbali za washiriki

Na: WMJJWM,Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. John Jingu amesema Serikali itahakikisha Wanawake hasa wa ngazi ya chini wanainuliwa katika nyanja zote ili kuchochea Usawa wa Kijinsia.

Dkt. Jingu amesema hayo wakati wa Kikao Kazi cha kujadili uwezeshaji kwa Wanawake nchini kilichoratibiwa na Benki ya Dunia ,Machi 22, 2023, na kufanyika Jijini Dar es salaam.

Amesema maazimio ya Kikao kazi hicho yatasaidia Mradi wa Benki ya Dunia ambao umejikita kuchochea ushirikishwaji na uwezeshaji wa wanawake kiuchumi.”Mradi wa PAMOJA”

“Ushiriki wetu kwenye kikao kazi hiki ni kiashiria tosha cha kujidhatiti kuleta Usawa wa Kijinsia nchini na kuhakikisha kunakua na Utekelezaji wa Afua zinazowekwa ili kuwainua Wanawake kiuchumi na kuondoa ukatili wa kijinsia” Amesema Dkt jingu.

Aidha, Dkt Jingu amesema Serikali ya Tanzania inatambua kwamba Usawa wa kijinsia ni muhimili muhimu katika kuleta Maendeleo ya Taifa na kusisitiza kuwa Usawa wa Kijinsia umebaki kuwa kipaumbele na ndiyo maana Serikali imesaini mikataba mbalimbali ya kimataifa inayolenga kuleta Usawa kwa huo.

“Kama mnavyojua Tanzania ilikua kati ya nchi zilizoshiriki wakati wa Jukwaa la Usawa (GEF ) na Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alikubali kusimamia Eneo la pili la kuhakikisha Taifa linafikia Usawa wa Kijinsia Hivyo Wizara inaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na Benki ya Dunia kuhakikasha Mradi huu unafanikiwa kwa Kufanya kazi kwa karibu na Wataalam mbalimbali kwenye Sekta zote muhimu”. Amesema Jingu.

Naye, Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt. Nandera Mhando amesema kuna haja ya Sheria zilizopo kuhakikisha zinamtetea Mwanamke kufanikisha masuala yanayomuhusu awapo kazini na baada ya kustaafu.

“Licha ya ushahidi wa maendeleo ya kiusawa wa Kijinsia tulio nao lakini bado Wanawake hawana fursa na Haki za Kiuchumi kama walizo nazo Wanaume. Usawa wa kijinsia siyo tu haki ya kibidamu bali ni Chachu ya msingi katika kuhakikisha Taifa linaendelea na kukua” Alisema Dkt Nandera.

Kwa Upande wake, Mtendaji Mkazi wa Benki ya Dunia, Nathan Belete amesema Benki hiyo itahakikisha inafanya kazi bega kwa bega na Serikali ya Tanzania ili kuhakikisha Usawa wa kijinsia unafikiwa kama ilivyokusudiwa na Rais wa Tanzania katika Jukwaa la Usawa kwa kuhakikisha kunakuwa na uwezeshaji na ushirikishwaji wa kiuchumi kwa wanawake.

Hali kadhalika, Mtaalam wa Masuala ya Wanawake, Biashara na Sheria kutoka Benki ya Dunia, Daniela Behr amesema kuna umuhimu wa Sheria zote kuangaliwa kwa umakini kwani usawa wa kijinsia ni ngumu kufikiwa kama Sheria zilizopo katika Nchi haziwezeshi wanawake kufikia Usawa huo.

MWISHO.

Previous articleSERIKALI NA SEKTA BINAFSI ZISHIRIKIANE KUINUA KILIMO
Next articleDKT. TAX AKUTANA NA BALOZI WA MAREKANI NCHINI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here