Home BUSINESS NHC YATOA SARUJI MIFUKO 75 KUSAIDIA UJENZI WA HOSTELI SINGIDA

NHC YATOA SARUJI MIFUKO 75 KUSAIDIA UJENZI WA HOSTELI SINGIDA

Meneja wa Shirika la Nyumb la Taifa (NHC) Mkoa wa Singida, Judith Mwalongo (kulia) kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa shirika hilo, akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Fadhili Chimsala, moja ya mfuko wa saruji kati ya 75 yenye thamani ya Sh. Milioni 1.5 iliyotolewa na shirika hilo kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa hosteli ya wasichana katika Sekondari ya Kintinku iliyopo wilayani Manyoni mkoani Singida leo hii Januari, 25, 2023. Wengine katikati ni dereva wa shirika hilo, Hassan Njiku na Afisa wa shirika hilo, Renalda Mlambo.

Na: Dotto Mwaibale, Manyoni

SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limetoa mifuko 75 ya saruji yenye thamani ya Sh. Milioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa hosteli ya wasichana katika Sekondari ya Kintinku iliyopo wilayani Manyoni mkoani Singida.

Akizungumza wakati akikabidhi saruji hiyo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Fadhili Chimsala kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo,  Meneja wa NHC Mkoa wa Singida, Judith Mwalongo alisema saruji hiyo ina kwenda kusaidia kukamilisha ujenzi wa hosteli hiyo na kuondoa adha ya kutembea umbali mrefu kwa wanafunzi wa shule hiyo wakati wa kwenda shuleni.

“Wanafunzi wa shule hii wanatembea umbali wa zaidi ya kilomita 10 kila siku wakati kwenda na kurudi nyumbani hali inayowafanya washindwe kupata masomo yao vizuri na sisi baada ya kuiona changamoto hiyo tukaamua kuchangia ujenzi wa hosteli hii” alisema Mwalongo.

Mwalongo alisema shirika hilo lina utaratibu wa kushiriki shughuli za kijamii kwa kusaidia katika  mambo ya maendeleo kama walivyofanya katika shule hiyo.

“Shirika letu lina utaratibu wa kurudisha faida tunayoipata kwa jamii kushiriki shughuli mbalimbali za maendeleo (Cooperate Social Responsibility) na leo tumekuja hapa Manyoni kushiriki ujenzi wa Hosteli katika Shule ya  Sekondari ya Kintinku kwa mara nyingine tena kwani tulishawahi kutoa msaada kama huu na yote hii ni kuunga mkono jitihada za Serikali za kusaidia shughuli za maendeleo” alisema Mwalongo.

Mwalongo alitoa ahadi ya kuendelea kusaidia ujenzi huo pindi watakapopata nafasi ya kufanya hivyo lengo likiwa ni kuhakikisha ujenzi wa hosteli hiyo unakamilika na wanafunzi wanaitumia.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Fadhili Chimsala akipokea msaada huo alilishukuru shirika hilo kwa msaada ambao wamekuwa wakiutoa mara kwa mara katika halmashauri hiyo na kuwa wamekuwa wadau wao wakubwa wa maendeleo.

“Kweli NHC mnafanya kazi kubwa katika halmashauri yetu hatuna maneno mengi zaidi ya kuwashukuru tunaomba hizi salamu zetu mtufikishie kwa mkurugenzi wenu mkuu Nehemia Mchechu na msichoke kutusaidia” alisema Chimsala. 

Meneja wa Shirika la Nyumb la Taifa (NHC) Mkoa wa Singida, Judith Mwalongo (kulia) na Afisa wa shirika hilo, Renalda Mlambo wakisaini fomu ya makabidhiano ya saruji hiyo.

Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Saida Moshi, akisaini fomu za makabidhiano ya saruji hiyo.
Picha ya pamoja baada ya makabidhiano ya saruji hiyo.
Previous articleRC SINGIDA AMWAGIZA DC IRAMBA KUWAKAMATA VIONGOZI WA CHAMA CHA AKIBA NA MIKOPO CHA CHAMWAI
Next articleSERIKALI YAAHIDI KUZIHAKIKI UPYA HOTELI ZA KITALII
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here