Home SPORTS BOCCO APIGA HAT-TRICK SIMBA IKIICHAPA RUVU SHOOTING 4-0

BOCCO APIGA HAT-TRICK SIMBA IKIICHAPA RUVU SHOOTING 4-0

Timu ya wekundu wa msimbazi Simba SC imeendeleza kichapo kwa kuitungua timu ya Ruvu Shooting kwa jumla ya mabao 4-0.

Katika mchezo huo uliopigwa leo Novemba 19,2022 katika Dimba la Mkapa Jijini Dar es Salaam, timu ya Simba SC ilipata mabao yake matatu katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo  mbapo magoli mawili yakifungwa na ‘Papaa’ John Bocco katika dakika ya 3, na 17 na goli la tatu likifungwa na  Shomari Kapombe  katika dakika ya 35 ya kipindi cha kwanza ya mchezo huo.

Kipindi cha pili John Bocco alifaniliwa kupiga hat-trick yake ya kwanza kwa kuipatia Simba bao la nne katika dakika ya 68 ya Kipindi cha pili kwa kumtambuka beki wa kati wa Ruvu Shooting na kupeleka mpira wavuni.

Kufuatia ushindi huo Simba wanakwenda kileleni na kuongoza Ligi ya NBC akiwa na jumla ya alama 27 na uwiano wa magoli 19 ya kufunga na kufungwa, huku Mabingwa watetezi timu ya Yanga ikishika nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi hiyo ikiwa na jumla ya alama 26 na uwiano wa magoli 13 ya kufunga na kufungwa.

Previous articleRAIS MHE.SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA KUFUNGUA MKUTANO WA MABALOZI WA TANZANIA UNAOFANYIKA ZANZIBAR TAREHE 19-2022
Next articleUZINDUZI WA CHANJO YA UVIKO-19 AWAMU YA PILI MKOANI MOROGORO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here