Home LOCAL BALOZI MBAROUK APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO BALOZI MTEULE WA DRC

BALOZI MBAROUK APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO BALOZI MTEULE WA DRC

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb.) amepokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi mteule wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) nchini, Mhe. Jean-Pierre Massala katika Ofisi za Makao Makuu ya Wizara tarehe 15 Novemba, 2022 Jijini Dodoma.

Akizungumza baada ya kupokea nakala hizo, Balozi Mbarouk amemhakikishia Balozi huyo kuwa Serikali itampa ushirikiano wakati wa utekelezaji wa majukumu yake hapa nchini

Balozi Mbarouk ameongeza kuwa Tanzania na DRC zitaendelea kushirikiana kwenye masuala mbalimbali yenye maslahi kwa pande zote mbili hususan biashara na uwekezaji.