Home LOCAL TASAC, WADAU WA USAFIRI KWA NJIA YA MAJI WATOA ELIMU KILWA

TASAC, WADAU WA USAFIRI KWA NJIA YA MAJI WATOA ELIMU KILWA

TASAC, wadau wa usafiri kwa njia ya maji watoa elimu Kilwa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi na Chukuzi, Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi-Zanzibar pamoja na wadau wengine wa Sekta ya Usafiri majini wametoa elimu kuhusu masuala mbalimbali yahusuyo usafiri kwa njia ya maji katika viunga mbalimbali vya Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi.

Wadau hao walitembelea na kutoa elimu kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika la TASAC, usalama wa abiria katika vyombo vya usafiri kwa njia ya maji, fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya usafiri kwa njia ya maji ikiwemo ufadhili wa masomo yanayohusu kesta hiyo ikiwa ni moja ya shughuli za kuadhimisha Siku ya Bahari Duniani. Wadau walitembelea Shule ya Sekondari Kilwa, Kivinje, Ilulu, Kikanda, mialo ya Kilwa Kivinje, Somanga pamoja na Kisiwa cha Songosongo na Nyuni.

Previous articleMAKALA MAALUM: UBORESHAJI SHERIA YA USALAMA BARABARANI ITAKAVYOPUNGUZA VIFO VITOKANAVYO NA AJALI
Next articleSHERIA YA USALAMA BARABARANI ILIVYO MWIBA KWA USALAMA WA WATOTO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here