Home LOCAL RAIS SAMIA AITISHA KIKAO CHA DHARURA KUJADILI KUPANDA KWA BEI YA MAFUTA...

RAIS SAMIA AITISHA KIKAO CHA DHARURA KUJADILI KUPANDA KWA BEI YA MAFUTA IKULU JIJINI DAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameitisha Kikao cha dharura usiku wa leo tarehe 08 Mei Ikulu ya Dar es Salaam kujadili tatizo la kupanda kwa bei ya mafuta nchini.

Miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati January Makamba, Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) Alphayo Kidata na makatibu wakuu wao.

Katika kikao hicho, Rais Samia amewaagiza viongozi hao kutafuta suluhisho la haraka  katika kukabiliana na tatizo hilo la Upandaji wa bei ya Mafuta nchini.

Previous articleRAIS SAMIA AZUNGUMZA KATIKA UZINDUZI WA FILAMU YA TANZANIA THE ROYAL TOUR JIJINI DAR ES SALAAM
Next articleKUTOKA MEZA YA MAGAZETI ASUBUHI YA LEO JUMATATU MEI 9-2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here