Home LOCAL RC MAKALLA: UJENZI WA SOKO UKIENDELEA ATAKA BARABARA ZA KUINGIA SOKONI ZIBAKI...

RC MAKALLA: UJENZI WA SOKO UKIENDELEA ATAKA BARABARA ZA KUINGIA SOKONI ZIBAKI WAZI

  • Ni Kufuatia Ufanyaji biashara kwenye eneo la Barabara na kumzuia
  • Mkandarasi kutekeleza majukumu.
  • Awataka kwenda kwenye maeneo waliyopangwa.
  • Maeneo yaliokatazwa kulindwa masaa 24.
Na: James Lyatuu, DAR ES SALAAM.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ameelekeza Halmashauri ya Jiji la Ilala kuimarisha ulinzi wa saa 24 kwenye Barabara za kuingia na kutoka linapojengwa Soko la kisasa Kariakoo kwa kuhakikisha zinapitika nyakati zote na kuwaonya Wafanyabiashara Wanaofanya biashara kwa kujiiba kwenye maeneo yaliyokatazwa.

RC Makalla amesema eneo la Karikoo linapojengwa Soko la kisasa kwa Sasa ni eneo hatarishi Kutokana na Shughuli za Ujenzi zinazoendelea hivyo amepiga marufuku Ufanyaji wa biashara kwenye eneo Hilo kwakuwa licha ya kuhatarisha usalama pia wanazuia Barabara ya magari yanayopeleka Vifaa vya Ujenzi na mitambo jambo linaloweza kufanya Ujenzi kuchelewa.
 
Akizungumza wakati wa zoezi la Usafi wa pamoja Wilaya ya Ilala ambapo Leo ameshiriki Usafi eneo la Karikoo, RC Makalla ametoa wito kwa Wafanyabiashara Wanaofanya biashara kwenye maeneo yaliyokatazwa kwenda kwenye maeneo waliyopangwa.

Aidha RC Makalla ameonyesha kukasirishwa na tabia ya baadha ya Watendaji wasiowaaminifu wanaopokea fedha (hongo) kutoka kwa Wafanyabiashara ili kuwaruhusu kufanya biashara kwenye maeneo yaliyokatazwa ambapo amewaonya Wafanyabiashara kujiepusha na hilo.

Pamoja na hayo RC Makalla amewatangazia Wafanyabiashara wanaodhani kuwa nafasi kwenye masoko zimejaa kuwa nafasi bado zipo hivyo wawasiliane na Mamlaka husika ili wapatiwe maeneo watakayofanya Biashara bila usumbufu.
 
Zoezi la Usafi eneo la Karikoo siku ya Leo limeenda sambamba pia na kuwapanga vizuri Wafanyabiashara waliokuwa wakifanya biashara kwenye maeneo yaliyokatazwa.


Previous articleSERIKALI YABORESHA HUDUMA ZA AFYA NZEGA MJI
Next articleRAIS WA UFARANSA EMMANUEL MACRON AMTUNUKU MEDALI YA KIMATAIFA MFANYABIASHARA MAARUFU TANZANIA JITESH LADWA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here