Home LOCAL SPIKA NDUGAI AMUOMBA RADHI RAIS SAMIA

SPIKA NDUGAI AMUOMBA RADHI RAIS SAMIA

Na: Mwandishi wetu, DODOMA.

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Job Ndugai amemuomba radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa namna moja au nyingine ametoa neno la kumvunja moyo kupitia uongozi wake.


Spika Ndugai ameyasema hayo leo Januari 3, 2022 katika mkutano wake na Waandishi wa habari Jijini Dodoma na 


“Binafsi yangu popote pale ambapo nilihisiwa labda kwa namna moja ama nyingine nimetoa neno la kumvunja moyo Rais wetu na akavunjika moyo nitumie fursa hii kumuomba radhi Mheshimiwa Rais na Watanzania wote, haliwezi kutokea halitotokea na sio rahisi jambo hilo kutokea, 


“Rais ndiye Kiongozi Mkuu, tumuheshimu pekee yake hatoweza tumsaidie kwasababu pamoja tunaweza kwenda mbali zaidi. Wabunge mtawasikia wapo na Rais, na sisi wote tunatekeleza sera na Ilani za CCM hatugombani hata siku moja, lakini wapo watu ambao wangependa kupita katikati na kutusambaratisha, Watu hao washindwe na walegee;


“Juzi tarehe 26 (Desemba 26,2021) nilikuwa kwenye shughuli nikazungumza baadhi ya mambo baadaye ikatengenezwa clip na baadhi ya watu wakakata baadhi ya mambo wakawasilisha ujumbe nusu ambao umesababisha mjadala mkubwa katika nchi yetu, mjadala ule umesababisha usumbufu wa hapa na pale nimeona tukutane pamoja na mambo mengine niweke sawa jambo hilo lilivyokuwa.


“Nyinyi waandishi mnaweza kufuatilia mkapata mkanda mzima, hapakuwa na jambo la kukashfu au kudharau juhudi zozote za Serikali, Serikali ni Baba yetu, Serikali ni Mama yetu tunahitaji Serikali na tunaiunga mkono,”amesema Mheshimiwa Ndugai.


Amesema kuwa katika mazungumzo hayo aliwataka wenzake pamoja na mambo mengine kujiimarisha kiuchumi, “tulipe kodi na tulipe tozo ili tuisaidie Serikali yetu katika kujitegemea zaidi na sisi kama nchi kujitegemea zaidi na nikaeleza kwa nini sisi Wabunge tulipitisha jambo hili la tozo na nikasema endapo wenzetu mnatuona Wabunge tulifanya jambo baya kupitisha jambo hili basi mtatuhukumu huko mbele, wabunge sikumaanisha taasisi nyingine yoyote,”amefafanua Mheshimiwa Ndugai.

Previous articleRANI YAIMWAGIA ZAWADI YANGA PRINCES
Next articleSERIKALI YAZINDUA CHANELI YA ELIMU ZANZIBAR TV (EZTV)
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here