Home LOCAL HEKAHEKA MAANDALIZI YA KUFUNGUA SHULE WANANCHI WALALAMIKIA KUPANDA KWA BEI ZA BIDHAA

HEKAHEKA MAANDALIZI YA KUFUNGUA SHULE WANANCHI WALALAMIKIA KUPANDA KWA BEI ZA BIDHAA

Mkazi wa Jiji la Dar es Salaam Amina Msafiri (kulia) akifanya manunuzi ya sare za shule Katika mtaa wa Kongo, kariakoo. (kushoto) ni mjasiriamali Ismail Abdullah.

Mzazi Gladis Heudi (kushoto) akimuonesha Shati binti yake (kulia) walipokuwa mtaa wa Kongo kariakoo Jijini Dar es Salaam kununua mahitaji mbalimbali ya bidhaa za Shule.

Mwenyekiti wa Umoja wa machinga Mkoa wa Dar es Salaam Namoto Yusuph akizungumza wakati wa mahojiano maalum. (PICHA: NA HUGHES DUGILO).

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.

Ikiwa imesalia siku moja wanafunzi kurudi shuleni, wananchi mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na viunga vyake wameendelea kufurika katika soko la machinga la mtaa wa Kongo kariakoo kwaajili ya kufanya maandalizi ya bidhaa mbalimbali za shuleni huku wakilalamikia kupandishwa bei za bidhaa hizo.

Baadhi ya wananchi walipoojiwa na Mwandishi wa Blog hii wamesema kuwa kumekuwa na tatizo la kupanda bei kwa bidhaa za shuleni kila ikifika wakati wa kufungua shule nakwamba swala hilo limekuwa kero kubwa kwao.

Gladis Heudi ni moja kati ya wazazi waliofika sokoni hapo na binti yake ili kumnunulia sare za shule huku akionesha kushangazwa na bei iliyopo.

“Kwakweli sina la kufanya inabidi nipunguze baadhi ya vitu ili ninunue kwanza sare maana bei zimepanda sana” anazungumza Gladis huku akonesha kusikitika.

 Kwa upande wake mzazi mwingine Amina Msafiri ameziomba Mamlaka husika kusimamia suala hilo kwani limekuwa likijirudia mara kwa mara na kusababisha usumbufu kwa wananchi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa machinga Mkoa wa Dar es Salaam Namoto Yusuph amesema kuwa lipo tatizo la baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu kupandisha bei za bidhaa hasa katika kipindi hiki cha kufunguliwa shele, hivyo kuwataka wananchi kuweka utaratibu wa kufanya maandalizi mapema ili kuepuka usumbufu huo.

“Ni kweli wapo baadhi yao wamekosa uaminifu na wanatumia fursa hii kupandisha bei za bidhaa jambo hili tunalifanyiakazi hasa kwa wafanyabiashara wenye maduka kuacha kupandisha bei kwani kwa kufanya hivyo inamlazimu machinga anaekutana na mlaji wa mwisho nayeye kupandisha ili apate faida” Amesema.

Aidha amezungumzia kuwepo kwa baadhi ya wazazi au walezi kwenda kwenye maeneo hayo na watoto wao jambo linalolowaletea usumbufu mkubwa kutokana na msongamano mkubwa uliopo nakwamba endapo watafanya maandalizi mapema wanakuwa wameepukana na usumbufu huo.
Previous articleKUTOKA MEZA YA MAGAZETI ASUBUHI YA LEO J. MOSI JANUARI 15-2022
Next articleMAJALIWA: UJENZI WA KIWANDA CHA MBOLEA CHA ITRACOM NI SAHIHI WAZIRI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here