Home LOCAL KAMANDA WA POLISI MKOANI IRINGA AFANYA OPARESHENI BARABARA KUU IRINGA -MOROGORO

KAMANDA WA POLISI MKOANI IRINGA AFANYA OPARESHENI BARABARA KUU IRINGA -MOROGORO

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa ACP Allan L. Bukumbi akiambatana na Mkuu wa Usalama Barabarani wamefanya Operesheni katika barabara kuu ya Morogoro – Iringa hususani eneo la Kitonga lakini pia kutoa elimu kwa Madereva ili kuepusha ajali zinazoweza kuzuilika hasa kipindi hiki cha Sikukuu za Mwisho wa Mwaka.

ACP Bukumbi amewakumbusha madereva kutii sheria za barabarani ili kuepuka ajali na kwamba hatosita kumchukulia hatua dereva yeyote atakaekiuka maadili ya udereva awapo barabarani.

Hali kadhalika Mkuu wa Usalama barabarani Mkoa wa Iringa, SP Yusuf Kamota ametumia muda huo kuwakumbusha kuwa Iringa sio sehemu sahihi kwa madereva wasiofuata sheria za barabarani na kwamba atahakikisha sheria zinatekelezwa ipasavyo.

Katika hatua nyingine, Kamanda Bukumbi amewataka abiria wawapo safarini, kutoa taarifa kwa wakuu wa usalama barabarani endapo kuna vitendo vya uvunjifu wa sheria kwani Jeshi la Polisi limeweka utaratibu wa kubandika mawasiliano kwenye Vyombo hivyo.

Previous articleNAMPUNGU WALALAMIKIA UBOVU WA BARABARA
Next articleKUTOKA MEZA YA MAGAZETI ASUBUHI YA LEO J.TATU DISEMBA 27-2021
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here