Home SPORTS PAWASA USHINDI LAZIMA DHIDI YA MSUMBIJI

PAWASA USHINDI LAZIMA DHIDI YA MSUMBIJI

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Na:Stella kessy

KIKOSI cha timu ya taifa ya soka la Ufukweni Tanzania  kesho wanashuka dimbani kuchuana na Msumbiji  katika  mashindano ya COSAFA yanayofanyika Durban, Afrika Kusini.

Akizungumza  kocha mkuu wa timu ya taifa ya soka la ufukweni Boniface Pawasa amesema kuwa kikosi kimejiandaa vyema kwa mchezo huo dhidi ya wapinzani wake Msumbiji

Amesema kuwa wachezaji wa morali ya ushindi kesho  katika mtanange huo na wachezaji wote wapo vizuri kuhakikisha wanapata ushindi.

Huku mchezo mwingine utakuwa kati ya Angola  dhidi ya Shelisheli na hii ni kutokana na Madagascar kujitoa katika michuano hiyo na kila kundi kubaki na timu tatu

Michuano hiyo imeanza leo huku South Afrika ikiibuka  na ushindi wa Mabao 4 – 2 dhidi  ya Shelisheli huku Msumbiji  wameichapa 8-3 Comoros