Home LOCAL HABARI PICHA:RAIS SAMIA ALIPOONDOKA JIJINI DODOMA NA KUWASILI NCHINI KENYA, LEO

HABARI PICHA:RAIS SAMIA ALIPOONDOKA JIJINI DODOMA NA KUWASILI NCHINI KENYA, LEO

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akishuka kwenye Ndege ya Tanzania baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi leo, kuanza ziara ya siku mbili nchini Kenya, akiwa nchini humo atakutana na kufanya mazungumzo na Mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, pia atahutubia Mabunge mawili ya Kenya na kuhutubia Mkutano wa Wafanyabiashara.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na wenyeji baada ya kushuka kwenye Ndege ya Tanzania alipowasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi leo, kuanza ziara ya siku mbili nchini Kenya.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisindikizwa baada ya kupokewa aliposhuka kwenye Ndege ya Tanzania baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi leo, kuanza ziara ya siku mbili nchini Kenya.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi leo, kuanza ziara ya siku mbili nchini Kenya.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiagana na baadhi ya viongozi wakati akienda kupanda Ndege kwenye Uwanja wa Ndege jijini Dodoma, kwenda nchini Kenya kuanza ziara ya siku mbili nchini humo, leo.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisindikizwa na Makamu wa Rais Dk. Isdori Philip Mpango wakati akienda kupanda Ndege kwenye Uwanja wa Ndege jijini Dodoma, kwenda nchini Kenya kuanza ziara ya siku mbili nchini humo, leo.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza mawili au matatu ya kuagana na Makamu wa Rais Dk. Isdori Philip Mpango, akiwa eneo la mapumziko mafupi wakati akisubiri kwenda kupanda Ndege kwenye Uwanja wa Ndege jijini Dodoma, kwenda nchini Kenya kuanza ziara ya siku mbili nchini humo, leo.

Previous articleCOVID-19: TANZANIA IMPOSES A 14-DAYS MANDATORY QUARANTINE FOR TRAVELLERS VISITING THE COUNTRY.
Next articleVIONGOZI WATAKIWA KUHAMASISHA WANANCHI KUPAMBANA NA MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here