Home SPORTS SIMBA YAENDELEZA UBABE KWA IHEFU, YAICHAPA 2-0 KWAO

SIMBA YAENDELEZA UBABE KWA IHEFU, YAICHAPA 2-0 KWAO

KLABU ya wekundu wa msimbazi Simba SC imefanikiwa kunyakua alama tatu muhimu kwa kuichapa timu ya Ihefu FC mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara uliochezwa katika Dimba la Highland Estates Mbarali Jijini MBEYA 

Magoli ya Simba yamepachikwa kambani na Jian Baleke katika dakika ya 83 na 89 za kipindi cha pili cha mchezo huo.

Baleke amekuwa mshambuliaji tegemeo katika Klabu ya Simba kutokana na umahili wake wa kupachika mabao ambapo kati ya magoli hayo aliyofunga katika mechi ya leo, moja amelifunga kwa tick-tack akimalizia mpira uliogonga mwambia.

Kufuatia matokeo hayo timu ya Simba SC inaendea kushika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi Kuu ya NBC ikiwa na alama 60 akibakiwa na michezo 4 kabla ya kumalizika kwa ligi hiyo.

Previous articleRAIS SAMIA APONGEZWA KUCHUKUA HATUA RIPOTI YA CAG
Next articleWAZIRI NAPE AFUTURISHA JIMBONI MTAMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here