Home LOCAL SERIKALI KUAJIRI WATAALAMU WA AFYA 12,000 MWAKA HUU.

SERIKALI KUAJIRI WATAALAMU WA AFYA 12,000 MWAKA HUU.

Na: WAF – Bungeni, Dodoma

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema, katika mwaka 2023 Serikali imepanga kuajiri Wataalamu wa afya 12,000, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuboresha huduma kwa wananchi hasa maeneo yenye upungufu wa Watumishi na kupunguza changamoto ya ajira kwa Wataalamu wa afya nchini.

Dkt. Mollel amesema hayo leo Aprili 12, 2023 Bungeni Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu Mhe. Minza Simon Mjika katika Mkutano wa 11 kikao cha tano,

Amesema, katika kuboresha huduma kwa wananchi katika kisiwa cha Ukerewe, Serikali imeipandisha hadhi iliyokuwa hospitali ya Wilaya hiyo na kuwa hospitali ya Mkoa, hali itayosaidia kuongezewa Wataalamu wa kutoa huduma, vifaa tiba na bajeti ya uendeshaji wa hospitali hiyo.

Aidha, Dkt. Mollel amesema, Wizara ya Afya itaendelea kushirikiana na OR TAMISEMI kuhakikisha mwananchi anapata huduma bora, kwa kuhakikisha maeneo yote yenye uhitaji hasa katika visiwa kunakuwa na zahanati katika kila kijiji na Wataalamu wa afya ili kupunguza kufuata huduma za afya kwa umbali mrefu.

Sambamba na hilo amesema, Serikali itaendelea kuwapanga watumishi katika Mikoa ya pembezoni mwa nchi kadri vibali vya ajira vitavyoendelea kutolewa kutokana na unyeti wa Mikoa hiyo kupakana na nchi nyingine hasa zenye milipuko ya magonjwa.

Mwisho.

Previous articleMAJINA YA KIGENI KUENDELEA KUTUMIKA KWA BAADHI YA RASILIMALI ZA TAIFA KULINDA HISTORIA NA UHIFADHI
Next articleMAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA MAJAJI MWANZA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here