Home BUSINESS NCT KUANZISHA MAFUNZO YA MUDA MFUPI YA URATIBU WA MATUKIO

NCT KUANZISHA MAFUNZO YA MUDA MFUPI YA URATIBU WA MATUKIO

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT), Taaluma, Tafiti, na Ushauri  Bi. Jesca William akizungumza alipokuwa akifungua mkutano kati Chuo hicho na wadau wa uratibu wa matukio uliofanyika leo April 12,2023 katika ukumbi wa Chuo hicho Jijini Dar es Salaam. 

Meneja Taaluma wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT), Mary Maduhu akizungumza alipokuwa akitoa salamu za utangulizi na kumkaribisha Makamu Mkuu wa Chuo hicho kuzungumza.

Mratibu wa Mafunzo ya Muda Mfupi wa NCT Francisco Juma akisoma ratiba ya shughuli hiyo na kutoa neno la ukaribisho katika kikao hicho.

Baadhi ya watumishi wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) wakiwa kwenye kikao hicho.

(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Na: Hghes Dugilo, DSM

Katika kuhakikisha kunakuwepo na ufanisi wa uratibu na usimamizi wa matukio, Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) kimeandaa Mafunzo ya muda mfupi na kuwakutanisha wadau mbalimbali katika tasnia hiyo kwa lengo la kuwatambulisha fursa zinazotolewa na chuo hicho katika kozi mbalimbali za muda mfupi wanazozitoa.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano kati ya Chuo hicho na wadau wa uratibu wa matukio, Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Taaluma, Tafiti, na ushauri Bi. Jesca william amesema lengo la kukutana na wadau hao ni kujadiliana kwa pamoja na kuangalia namna ya kuwajenga uwezo zaidi pamoja na kujua mahitaji halisi ya tasnia hiyo sambamba na kuendelea kutoa mafunzo itakayoendana na mahitaji halisi ya soko la sasa.

Amesema NCT inatambua kuwa tasnia hiyo inakuwa kwa haraka na kutoa mchango mkubwa kwa wadau wa tasnia hiyo katika kukuza utalii na kutoa fursa kwa vijana kujiajiri na kuchangia kukuza uchumi wa mtu binafsi  na Taifa kwa ujumla.

“Naomba kutoa rai kwa Viajana kujiunga na kozi ya Uratibuwa matukio ambayo inatolewa katika Chuo chetu cha Taifa cha Utalii Kampasi ya Bustani” amesema Jesca.

Na kuongeza kuwa “Ni matarajio ya Chuo kuwa wadau mbalimbali watajitokeza kuchangamkia fursa hii ya mafunzo yanayotolewa kwa kushirikiana na Wadau wa tasnia hii ili kuhakiksha washiriki wanapata ujuzi stahiki unaoendana na Soko la sasa la kuratibu na kuendesha shughuli hizi kitalaam zaidi”  Ameongeza.

Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakizungumza kwa nyakati tofauti walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari wamepongeza uongozi wa chuo hicho kwa kuendesha mafunzo hayo, ambapo Msanii maarufu wa maigizo nchini (Dkt. Cheni) amesema mafunzo hayo yatakwenda kuwaongezea ujuzi ambapo sasa wanakwenda kufanyakazi zao kitaalam.

“Chuo hiki kimekuwa msaada mkubwa kwetu, kwa kuandaa mafunzo haya sasa tunakwenda kufanya shughuli zetu kitaalam zaidi, tunapongeza Uongozi wa Chuo cha Taifa cha utalii kwa kuandaa mafunzo haya” amesema Dkt. Cheni.

Tasnia ya Uratibu wa Matukio ni Sekta inayohusisha watu mbalimbali wakiwemo, Waratibu wa Matukio katika taasisi na watu Binafsi (Events Planners), Waandaaji wa Mikutano mbalimbali (Conference Organizers), Waratibu wa Matamasha mbalimbali, Waratibu wa matukio ya Kitamaduni (Cultural Events), Washereheshaji (MCs), Wapambaji, Wapishi na wadau wengine. 

(PICHA MBALIMBALI ZA WADAU KATIKA KIKAO HICHO)

Previous articleWATU 400 KUFANYIWA UPASUAJI WA MTOTO WA JICHO-MBARALI
Next articleCHIKOTA:NANYAMBA KUNA UPUNGUFU WA WATUMISHI WA AFYA 610
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here