Home BUSINESS WAMILIKI WA KAMPUNI WATAKIWA KUWA WAADILIFU

WAMILIKI WA KAMPUNI WATAKIWA KUWA WAADILIFU

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), imewataka wamiliki wa Kampuni nchini, hususani zile zinazo shirikiana na kampuni za kigeni kuzingatia maadili katika utendaji kazi wao ili kuepuka udanganyifu wa aina yoyote kwa wateja wanaowahudimia.

Kauli hiyo imetolewa Machi 16, 2023 na Kaimu Mkurugenzi wa Makampuni na Majina ya Biashara wa BRELA, Bw. Mainrad Rweyemamu katika warsha ya Uhamasishaji na Utekelezaji wa Kanuni za Wamiliki Manufaa wa Kampuni kwa Washauri wa Biashara, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Amboseli Kapripoint Jijini Mwanza.

Bw. Rweyemamu amesema baadhi ya kampuni zinazoshirikiana na kampuni za nje zimekuwa zikifanya kazi bila kuzingatia uadilifu katika kuwahudumia wateja, hivyo kutakiwa kufuata sheria na taratibu za mikataba ya usajili ikiwa ni pamoja na kufuata taratibu katika fomu ya uadilifu.

“Fomu hiyo itawasaidia kujihadhari dhidi ya vitendo vya rushwa, kuepuka dhuluma katika kampuni na kuhakikisha wanafanya kazi vizuri ili kufikia malengo ”, amesema Bw. Rweyemamu

Aidha amesema kampuni za nje ni kichocheo kikubwa cha uchumi nchini, ambapo zimekuwa zikilisaidia taifa kuingiza fedha za kigeni na kuongeza wigo wa ajira, hivyo kwa kuzingatia uaadilifu taifa litafaidika zaidi.

Hata hivyo ameongeza kuwa ili kuepuka kampuni yoyote kufutiwa Usajili na Msajili wa Makampuni nchini ni vyema wakafuata matakwa ya kuanzishwa kwa Kampuni husika.

Vilevile amewataka watanzania kuhakikisha kabla ya kuanzisha kampuni kuwa na ufahamu kuhusu uendenshaji wake na kujua matakwa ya kisheria.

“Mmiliki wa Kampuni yoyote lazima awe na taarifa sahihi na kwa wakati ili zinapohitajika zipatikane na sio anakuwa mmiliki jina kama ambavyo baadhi ya kampuni zinavyofanya kazi na kusababisha kukosa vigezo”, amesisitiza Bw. Rweyemamu.

Kwa upande wake Bw. Steven Kitale ambaye ni Wakili wakujitegemea na mshauri wa moja ya kampuni mkoani Mwanza, amesema kufuatia mafunzo hayo wamepata uelewa kuhusu mfumo mzima wa kampuni na namna wamiliki wanavyotakiwa kuwa katika kampuni zao, huku akiongeza kuwa BRELA waendelee na elimu hii mara kwa mara ili kampuni nyingi zukumbuke wajibu wao.

BRELA imekuwa ikifanya mafunzo haya ya Miliki Manufaa katika mikoa mbalimbali na kusikiliza changamoto za wadau mbalimbali pamoja na kutoa msaada wa papo kwa papo.

Previous articleBRELA KUCHOCHEA UJIO WA WAWEKEZAJI NCHINI
Next articleWAZIRI MKUU ATOA MKONO WA POLE KWA KATIBU MKUU JIM YONAZI KWA KUFIWA NA MDOGO WAKE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here