Home SPORTS TAIFA STARS MGUU SAWA KUFUZU AFCON, YAILAZA UGANDA 1-0

TAIFA STARS MGUU SAWA KUFUZU AFCON, YAILAZA UGANDA 1-0

Timu ya soka ya Tanzania (Taifa Stars) imeijiweka sawa kufuzu kucheza michuano ya AFCON kwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda (The Crains) katika mchezo wa kufuzu kucheza michuano hiyo uliopigwa katika Jiji la Ismailia nchini Misri.

Goli la Stars lilipatikana katika kipindi cha pili cha mchezo huo likifungwa na mshambuliaji wake Simon Msuva kwa shuti lililomshinda mlinda mlango wa Uganda.

Kufuatia matokeo hayo Taifa Stars inashika nafasi ya 2 ya msimamo wa kundi F ikiwa na alama 4 nyuma ya Algeria wenye alama 9 ikifuatia Niger wenye alama 2 huku Uganda ikishika mkia ikiwa na alama 1.

Baada ya mchezo huuo Taifa Stars wanatarajia kurejea nyumbani Tanzania siku ya kesho Machi 25 kujiandaa na mchezo wa marudiano utakaochezwa Machi 28 katika Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es salaam.

Iumbukwe kuwa Taifa Stars imeshakuta mara 11 na Uganda huku Uganda wenyewe wakishinda mara 4 na Stars mara 4 na kutoka sare mara 3

Previous articleTUUNGANE KUTOKOMEZA KIFUA KIKUU – WAZIRI MKUU
Next articleOFISI YA MAKAMU WA RAIS KUANZISHA KITUO CHA NYARAKA ZA MUUNGANO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here