Home SPORTS SHABIKI WA SIMBA : HOROYA FC WATUSAMEHE TU, LEO HAWATOKI KWA MPAKA

SHABIKI WA SIMBA : HOROYA FC WATUSAMEHE TU, LEO HAWATOKI KWA MPAKA

Na: Tima Sultan , DAR ES SALAAM 

SHABIKI na Mwanachama wa Klabu ya Simba, Michael Charles Magige, amewataka Horoya FC kuwasamehe kwani lazima leo wata waharibia malengo yao kwakuwafunga kwenye Uwanja wa Mkapa nakuweka Historia nyingine ya kuingia hatua ya Robo fainali michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika.

Simba leo saa 1:00 usiku wanatarajia kushuka kwenye Dimba hilo na kupepetuana na Kikosi hicho cha Horoya kutoka nchini Guinea kuitafuta tiketi ya kuingia robofainali kwenye mashindano hayo ya kimataifa.

Magige ni mwanachama hai wa Tawi la Simba Plutnum lililopo Teme, Jijini Dar es Salaam, ameyazungumza hayo akiwa uwanjani hapo akisubiria mchezo wao uanze.

Amesema anamshukuru Mwenyezi Mungu Kwa kumfikisha siku ya leo
kuweza kuwa sehemu ya mashuhuda wa historia ambayo muda sio mrefu inaenda kuwekwa na timu yake pendwa
Simba Sport Club.

Michael amesema anaiamini mno n timu yake kuw wana wachezaji wazuri ambao wameamua kucheza kwa faida ya timu basi wapinzani wao Horoya hawana budi kuwasamahe nilazima waingie robo fainali.

“Ninawaamini sana wachezaji wangu ninaamini pia kwa viongozi wangu wa klabu pia ninaamini na Mashabiki wenzangu wanachama na wale wote wenye kuitakia Mema timu yetu pendwa ki mtazamo mchezo utakuwa mgumu sana kwa kuwa ni wa kuamua hatma ya nani aende Robo Fainali,” alisema

Previous articleNENDENI MKASIMAMIE AJENDA ZA KITAIFA – MAJALIWA
Next articleDIWANI WA KIPAWA AMEWASHAURI WAZAZI KUCHANGIA CHAKULA CHA WANAFUNZI SHULENI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here