Home SPORTS MWANA FA AZINDUA RASMI RADHAN CUP, SILENT OCEAN IKIILAZA DISCOUNT FC 1-0...

MWANA FA AZINDUA RASMI RADHAN CUP, SILENT OCEAN IKIILAZA DISCOUNT FC 1-0 MCHEZO WA UFUNGUZI

NA: TIMA SULTANI

NAIBU Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ( MWANA FA) ambaye ni mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Mashindano ya Ramadhani Cup 2023 amewapongeza Silent Ocean kwa kuandaa mashindano hayo makubwa yenye lengo la kuibua vipaji vya wachezaji wasoka.

Naibu Waziri ameyazungumza hayo kwenye uzinduzi wa mashindano hayo uliofanyika usiku wa machi 27 kwenye Uwanja wa JMK Park, Jijini Dar es Salaam

Mchezo wa kwanza wa mashindano hayo ulimalizika kwa Silent Ocean FC kushinda bao 1-0 dhidi ya Discount FC ambao umechezwa saa 5:00 usiku.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo Naibu Waziri, Hamis Mwinjuma amewashukuru waandaaji wa mashindano hayo Silent Ocean. kwakumpa nafasi yakuwa mgeni rasmi aliwahi kuhudhuria kipindi chanyuma lakini anaona kipindi hiki yamekuwa tofauti sana 

Amesema kubwa kabisa lililomfurahisha nikufungua kwa mashindano hayo wakati timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inaingia uwanjani kuvaana na Uganda.

Naibu waziri huyo amesisitiza kuwa wao kama wapenzi wampira miongoni mwa jambo ambalo wanaweza kulifanya nikuwa wachezaji waku12 nakuwasapoti Stars katika kipindi chote.

“Mh Rais Samia Suluhu Hassan amenunu Tiketi 7000 huku Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akinunua tiketi 2000 hizo zote nijuhudi zakuhakikisha watu wanaend uwanjani bure hakuna anayetakiwa kukosa.

“Silent Ocean leo wameongeza tiketi 3000 na K4S Security wameongeza tiketi 1000 jumla 4000 hivyo amewataka na Yanga kuongeza tiketi 500 kati ya zile 1500 ambazo waliongeza mwanzo n Rais wa klabu hiyo ameongeza 500 ,” amesema

Aidha amekiri kuwa nafuraha kwa kupewa heshima hiyo kubwa kwenye ramadhani Cup 2023 anaamini kwa walivyojipanga inakwenda kuwa yakipekeee na alivipongeza vilabu vyote ambavyo vimejitokeza kushiriki mashindano hayo.

Naye Mtendaji Mkuu wa Silent Ocean, Mohamed Sokola, amesema kwaniaba yakampuni yao wanashukuru timu zote zilizojitokeza kwenye mashindano hayo.

“Kabla yakuanza mashindano kulikuwa nachangamoto nyingi tunaomba radhi lengo lilikuwa nikuyafanya yawe bora zaidi tunaamini mashindano haya yatakuwa mazuri kwani yanashuhurikiwa nawatu wa mpira ambao ni Chama Cha Soka Cha Mpira wa Miguu Dar es Salaam ( DRFA) ,” amesema Mohamed Soloka.

Previous articleTANZANIA NA INDIA KUENDELEZA UHUSIANO WA KIBIASHARA NA UWEKEZAJI 
Next articleYASEMAVYO MAGAZETI YA LEO JUMANNE MACHI 28,2023
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here