Home SPORTS FREDERICO WA SINGIDA BIG STARS AONGEZEWA MUDA WA UANGALIZI

FREDERICO WA SINGIDA BIG STARS AONGEZEWA MUDA WA UANGALIZI

MCHEZAJI wa Singida Big Stars Dario Frederico, amemaliza likizo yake ya mwezi mmoja na ripoti ya daktari inaonesha amepona kwa zaidi ya 90%.

Hata hivyo, klabu kupitia kwa ushauri wa kitaalamu wa daktari imemuongezea muda Dario Jr ili aweze kuwa timamu kwa 100% apate na muda wa kutosha wa kupumzika.

Kutokana na maamuzi haya, mchezaji huyo raia wa Brazil ataungana na kikosi rasmi wakati wa maandalizi ya ligi kuu msimu ujao wa 2023/24.

Wadau na mashabiki wa Singida Big Stars watarajie kumuona Dario akiwa kwenye kiwango bora zaidi atakapoungana na timu kwenye kambi yetu ya Pre-season nchini Tunisia.

Taarifa hiyo imetolewa hivi karibuni na Ofisa Habari wa klabu hiyo, Hussein Masanza.

Previous articleTGNP NA DIT KUJA NA SULUHISHO LA MASUALA YA JINSIA KWA NJIA YA KIDIJITALI
Next articleKAGERA NI SHWARI HAKUNA MAAMBUKIZI MAPYA YA UGONJWA WA MARBURG
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here