Home BUSINESS DC ILALA AZINDUA MSIMU WA GS1 BARCODES DAY 2023

DC ILALA AZINDUA MSIMU WA GS1 BARCODES DAY 2023

#Barcodes Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amezindua Msimu wa GS1 Tanzania wa Barcodes Day 2023 Itakayofanyika kuanzia Tarehe 15 hadi 19 June 2023 utakaokwenda sambamba na “Operesheni Ibua viwanda” pamoja na kuhamasisha kampeni ya “Buy Tanzania Buy 620”. Msimu huo umelenga katika kuhamasisha matumizi ya Kidigital kwa SMEs za Tanzania.

Kazi kubwa ya GS1 ni utoajiwa huduma za Barcodes, ambapo kwa mwaka huu taasisi hiyo imejipanga katika kuhakikisha, viwanda vyote vilivyopewa Barcodes vinachukua nafasi kubwa katika kuongeza uzalishaji na kuongeza ajira kwa wananchi nchini.

GS1 Beyond Barcodes 2023 imejikita katika kuhakikisha taasisi ya GS1 Tanzana inaunganisha nguvu na wadau wengine katika, kujenga mfumo wa viwanda vyenye matokeo makubwa kwa ajili ya kujenga Sekta Binafsi Imara.

GS1 Tanzania mwaka huu imepania kusimamia upelekaji wa Bidhaa za Viwanda vyenye Barcodes nje ya nchi ili kupata masoko ya kimkakati, GS1 Tanzania Barcodes Day inakwenda kuleta mabadiliko katika kuzitambulisha bidhaa za wazalishaji, wenye Barcodes kwa ajili ya matokeo makubwa.

Previous articleWIZARA YA AFYA YAKUTANA NA KAMATI YA BUNGE DODOMA
Next articleSERIKALI KUENDELEA KUIMARISHA MAZINGIRA WEZESHI YA WAJASIRIAMALI – MHE. KIGAHE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here