Home LOCAL WAVAMIA KANISANI NA KUFANYA UHARIBIFU GEITA 

WAVAMIA KANISANI NA KUFANYA UHARIBIFU GEITA 

Watu wawili wanashikiliwa na Jeshi la polisi Mkoani Geita kwa tuhuma za kuvamia Kanisa Kuu la Kiaskofu Jimbo Katoliki la Geita usiku wa kuamkia leo ambapo wamevunja mlango na kuingia ndani kisha kuharibu vitu vitakatifu vikiwemo mavazi ya misa na kuvunja misalaba.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita ACP Berthaneema Mlayi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo amesema mpaka sasa watu wawili wanashikiliwa na Jeshi hilo kwa ajili ya upepelezi wa tukio hilo.

“Hadi sasa, Polisi tunawashikilia watu wawili kwa mahojiano akiwemo mlinzi aliyekuwa zamu usiku wa tukio. Taarifa zaidi nitazitoa kesho,” amesema Kaimu Kamanda Mlay”

Kwa mujibu wa Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Geita, Flavian Kasala, amesema uvamizi na uharibifu uliofanyika umesababisha hasara ya zaidi ya Sh20 milioni pamoja na kuleta madhara ya kiimani.

Askofu Kasala amesema mtu huyo aliyejipenyeza ndani ya eneo la Kanisa kwa kuvunja kioo cha lango kuu pia amevunjavunja eneo la kuhifadhia sakramenti.

Askofu Kasala amesema kijana huyo ambaye tayari anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano ameharibu kiti cha Kiaskofu, chumba cha ambacho Maskofu na Mpadre wanafanyia maandalizi kabla ya ibada.

“Mtu huyo ambaye hadi sasa hatujafahamu sababu za uvamizi wake pia aliharibu kwa kuvunja vitu na vifaa mbalimbali ikiwemo misalaba, sanamu za kiimani na vyombo vya kuhifadhia maji ya Baraka ambayo pia aliyamwaga,” alisema Askofu Kasala

Kwa Mjibu wa Askofu Kasala amesema kabla ya kuhalibu kuharibu mali na samani za Kanisa, kijana huyo aling’oa kamera za ulinzi na usalama na kuharibu kifaa cha kuhifadhi kumbukumbu za matukio.

“Uvamizi na uharibifu uliofanyika siyo tu umesababisha madhara ya kiimani, bali pia hasara inayokadiriwa kuwa zaidi ya Sh20 milioni,” amesema Askofu Kasala

Previous articleDKT. TAX APOKEA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO ZA MABALOZI WA ZAMBIA BRAZIL NA VATICAN
Next articleMPOGOLO ATOA MIKAKATI KUIENZI BARABARA YA LUMUMBA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here