Home LOCAL TMDA YAPATA TUZO YA UBORA KATIKA KUELIMISHA JAMII

TMDA YAPATA TUZO YA UBORA KATIKA KUELIMISHA JAMII

Meneja wa TMDA Kanda ya Mashariki Bw. Adonis Bitegeko (kwanza kushoto) akipokea Tuzo ya kutambuliwa kuwa Taasisi Bora katika Uelimishaji Jamii kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TMDA. Tuzo hiyo imekabidhiwa na  Rais wa Chama cha Maafisa Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma Tanzania Assah Mwambene (wa pili kulia) katika hafla iliyofanyika Februari 18, 2023 Jijini Dar es Salaam. (wa kwanza kulia) ni  Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TMDA Schola Njozi, na (katikati) ni, Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa Taasisi hiyo Roberta Feruzi.

Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Roberta Feruzi akiwa ameshika Tuzo hiyo mara baada ya kumalizika kwa hafla hiyo Februari 17,2023 Jijini Dar es Salaam.

Meneja wa TMDA Kanda ya Mashariki Bw. Adonis Bitegeko (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Maafisa Mawasiliano waandamizi wa Taasisi hiyo, Roberta Feruzi (kushoto), na Schola Njozi (kulia) mara baada ya kumalizika kwa hafla hiyo Jijini Dar es Salaam.

Meneja wa TMDA Kanda ya Mashariki Bw. Adonis Bitegeko (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya wawakilishi wa Taasisi zilizopata Tuzo katika hafla hiyo. (wa pili kulia), ni Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TMDA Roberta Feruz.

Previous articleTASAF YAPUNGUZA UNYANYASAJI WA KIJINSIA KWA WANAWAKE BUNDA, KUJIAMINI KWAONGEZEKA
Next articleYANGA SC YAONDOKA NA MILIONI 15 ZA RAIS SAMIA IKIICHAPA TP MAZEMBE 3-1 KWA MKAPA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here