Home SPORTS SIMBA YAFUFUA MATUMAINI CUF, YAICHAPA VIPERS 1-0 KWAO

SIMBA YAFUFUA MATUMAINI CUF, YAICHAPA VIPERS 1-0 KWAO

Timu ya wekundu wa msimbazi Simba SC imefanikiwa kupata ushindi wake wa kwanza katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika kwa kuichapa timu ya Vipers ya Uganda bao 1-0 mchezo uliopigwa leo Februari 25, 2023 Jijini Kampala nchini Uganda.

Goli la Simba lilipachikwa kambani na mlinzi wa Kati wa timu hiyo Frank Inonga  katika Kipindi cha kwanza cha mchezo huo.

Kipindi cha pili timu zote zilirudi uwanjani na kucheza kwa kasi huku Kila timu ikifanya mabadiliko ambapo kwa upande wa Simba walimpumzisha Patrick Phil na nafasi yake kuchukuliwa na Erasto Nyoni, na Abibu Kyombo akiingia kuchukua nafasi ya Kibu Denis.

Pia Clatus Chama alipumzika na nafasi yake kuchukuliwa na Kennedy Juma katika dakika za lala salama za mchezo huo.

Kufuatia matokeo hayo timu ya Simba inapanda hadi nafasi ya tatu ya msimamo wa Kundi lao ikiwa nyuma ya holoya.

Previous articleTANTRADE, WADAU WAKUTANA KATIKA MDAHALO MAALUM JIJINI DAR
Next articleJUMUIYA YA WAZAZI DSM YAUNDA KAMATI NDOGO ZA JUMUIYA HIYO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here