Home LOCAL JUMUIYA YA WAZAZI DSM YAUNDA KAMATI NDOGO ZA JUMUIYA HIYO

JUMUIYA YA WAZAZI DSM YAUNDA KAMATI NDOGO ZA JUMUIYA HIYO

Mwenyekitiwa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar esSalaam, Khadija Ally Said akimkabidhi barua Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Dares Salaam, Walid Alhad ya kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya naMalezi kwenye Jumuiya hiyo wakati wa hafla fupi iliofanyika leo jijiniDar es salaam.

Mwenyekitiwa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar esSalaam, Khadija Ally Said akimkabidhi barua Ndugu Mjumbe wa Kamati yaElimu, Afya na Malezi Bw.Ismail Sadick (Suma Lee) kwenye Jumuiya hiyowakati wa hafla fupi iliofanyika leo jijini Dar es salaam.

Mwenyekitiwa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar esSalaam, Khadija Ally Said akimkabidhi barua Ndugu David Minja ya kuwaMwenyekiti wa kamati ya uchumi wa Jumuiya hiyo wakati wa hafla fupiiliofanyika leo jijini Dar es salaam.

Mwenyekitiwa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar esSalaam, Khadija Ally Said akizungumza wakati  Jumuiya hiyo kukamilishakuunda Kamati ndogo za Jumuiya hiyo ili kuhakikisha  inakuwa dira yamkoa na inayokwenda kusimamiwa ndani ya miaka mitano katikakutekeleza na kusimamia mipango kazi ambayo imejiwekea 

Mwenyekiti wa kamati ya uchumi wa Jumuiya ya  Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu David Minja akizungumza jambo mara baada ya kuteuliwa kwenye kamati ndogo mojawapo katika jumuiya hiyo .

Na: Mwandishi Wetu, Dar es Salaam 
 
JUMUIYA ya Wazazi  ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar ea Salaam imeunda Kamati ndogo za Jumuiya hiyo ili kuweza kuhakikisha Jumuiya ya Wazazi ya mkoa huo inakuwa dira ya mkoa na inayokwenda kusimamiwa na kuhakikisha inatekeleza na kusimamia mipango kazi ambayo wamejiwekea kwa miaka mitano.
 
Akizungumza katika hafla ya kuwakabidhi barua za uteuzi Wanakamati, leo Februri 25, 2023 jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Mkoa Dar ea Salaam, Bi. Khadija Ally Said amesema anategemea ushirikiano mkubwa kutoka kwenye Kamati zilizoundwa na kuhakikisha kazi za Jumuiya ya wazazi ndani ya mkoa wa Dar es salaam zinafanyika vizuri.
 
Kamati ambazo zimeundwa na kutangazwa ni Kamati tano ambazo ni Kamati ya Miradi, Uchumi na Maendeleo, Kamati ya Utamaduni, Michezo na Mazingira, Kamati ya Elimu, Afya na Malezi, Kamati ya Nidhamu na Maadili pamoja na Kamati ya Habari za Jumuiya.
 
Kuhusu Kamati ya Elimu, Afya na Malezi, Bi. Khadija amesema wao kama Jumuiya
ya Wazazi, malezi ni ajenda yao kitaifa, ndiyo maana wanakuja na Kaulimbiu ya ‘Malezi bora kwa Mtoto’, Faraja ya Kesho ya Mzazi na Taifa’, ambapo Kamati hiyo ina Wataalamu ambao wataenda kufanya mafunzo kwa viongozi wa ngazi ya kata, pia Kamati hiyo ina viongozi wa kiroho.
 
“Kamati hii inaenda kusimamia mambo ya msingi sana ya malezi na maadili lakini pia suala zima la elimu kuhakikisha ufaulu wa Mkoa wa Dar es Salaam wa
Watoto wa Shule za Msingi na Sekondari unaongezeka, lakini tunaenda kuanzisha Shule za awali ambayo kupitia hii Kamati wataweza kutuanzishiaumuhimu wa Shule za awali katika ngazi ya Kata, Wilaya lakini kuhakikisha kwamba jumuiya ya wazazi inasimamia Elimu katika ubora wake na afya vilevile,” amesema Bi. Khadija 
 
Aidha, Bi. Khadija amesema Kamati ya Miradi, Uchumi na Maendeleo inaenda kusaidia kwa kiwango kikubwa ndani ya mkoa kwani katika sera za Siasa na Uchumi lazima kuwe na Miradi ambayo iko katika hali sahihi na watafanya kazi katika miradi ambayo Jumuiya ya Wazazi itaweza kubuni.
 
Pia amesema kusimamia na kuiongoza kuhakikisha wanabadilisha hali ya wanajumuiya wake katika ngazi ya Kata, Wilaya na Mkoa lakini pia kufanya miradi ambayo inapeleka jumuiya na Chama cha Mapinduzi moja kwa moja na wananchi katika kuongeza kipato chao.
 
Pamoja na hayo, miongoni mwa Kamati ambazo zimeundwa, kuhusu Kamati ya
Utamduni, Michezo na Mazingira, amesema kuwa katika kujenga mahusiano yetu lazima tuingie kwenye michezo, kwahiyo watakuwa na timu za wazazi katika kata zao, watakuwa na mashindano ya michezo mbalimbali katika kata, wilaya na katika ngazi ya mkoa.
 
“Tunategemea kama tukifanya vizuri kuingia na kwenda hata nje ya nchi kupitia timu zetu , na hii ni kwaajili ya kupanua wigo wa mahusiano kati ya Chama lakini pia na wananchi wake kwahiyo michezo ndio sehemu peke yake watu wanakutana kwa pamoja”,
 
“Na sisi jumuiya ya wazazi tutafanya kazi na mtu yoyote mwenye nia njema naTanzania, hasa katika kuhakikisha malezi ya watoto na vijana wetu yanapewa kipaumbele. Ndio maana kamati hizi zimejumuisha makundimbalimbali ya kijamii, sio kamati za kishabiki.” amesema Bi. Khadija
 
Kwa upande wake, Mjumbe wa Kamati ya ya Elimu, Afya na Malezi, Bw. Ismail Sadick (Suma Lee) amesema atajitahidi kushirikiana na wajumbe wengine kuhakikisha suala la elimu na malezi linakuwa bora katika Mkoa wa Dar es
Salaam kwasababu katika Kamati hiyo wapo viongozi wa kiimani ambao pia
ataenda kushirikiana nao
.
Previous articleSIMBA YAFUFUA MATUMAINI CUF, YAICHAPA VIPERS 1-0 KWAO
Next articleWENYE ULEMAVU WAOMBA GHARAMA ZA VITI MWENDO ZIPUNGUZWE, DKT. MOLLEL AWAONDOA SHAKA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here