Home SPORTS SIMBA SC YAIZAMISHA MBEYA CITY 3-2 KWA MKAPA

SIMBA SC YAIZAMISHA MBEYA CITY 3-2 KWA MKAPA

Klabu ya Soka ya wekundu wa Msimbazi Simba SC imeichapa timu ya Mbeya City  jumla ya mabao 3-2 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara uliopigwa katika Dimba la Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Simba ilipata bao la kuongoza katika dakika ya 10 ya mchezo huo likipachikwa na Saidoo Ntibanzokiza akiunganisha pasi safi kutoka kwa Clatus Chama.

Dakika tatu baadaye Mbeya City walisawazisha goli hilo kupitia kwa Richard Ngodya kwa mpira wa adhabu ikiwa ni dakika ya 13 ya mchezo huo.

Saidoo Ntibanzokiza tena alipachika bao la pili kwa mkwaju wa penati katika dakika ya  49 ya mchezo huo, huku Pape Othman Sakho akipigilia msumali wa 3 dakika ya 55 ya kipindi cha pili kwa shuti kali baada ya kupokea pasi kutoka kwa Saidoo Ntibanzokiza.

Hata hivyo timu ya Mbeya City ilipata bao lake la pili kupitia mchezaji wake Juma shemvuni katika dakika ya 78 ya mchezo huo.

kufuatia matokeo hayo timu ya Simba SC inaendelea kushikilia nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Ku ya NBC ikiwa na alama 47 ikiwa nyuma ya watani wao wa jadi Young Africans yenye alama 53.

Previous articleWAKURUGENZI MKOA WA SINGIDA WAPEWA DESA LA KUONGEZA MAPATO
Next articleTAASISI ZINAZOENDELEA NA UJENZI WA OFISI ZATAKIWA KUKAMILISHA MAJENGO YAO KWA WAKATI JIJINI DODOMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here