Home LOCAL RAIS SAMIA ARIDHIA TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA 77 WA KAMISHENI...

RAIS SAMIA ARIDHIA TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA 77 WA KAMISHENI YA UMOJA WA AFRIKA WA HAKI ZA BINADAMU NA WATU

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu Mhe. Prof. Remy Ngoy Lumbu alipofika Ikule ya DSM leo 30/01/2023.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu Mhe. Prof. Remy Ngoy Lumbu.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu Mhe. Prof. Remy Ngoy Lumbu, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Damas Ndumbaro na viongozi wengine kutoka Wizara ya Katiba na Sheria na asasi za kiraia za watetezi wa haki za binadamu.

Na: Lusajo Mwakabuku – WKS

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi lililotolewa na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu Mhe. Prof. Remy Ngoy Lumbu la kuitaka nchi ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa 77 utakaojumuisha nchi wanachama wa kamisheni ya Umoja wa Afrika wa Haki za Binadamu na watu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Rais Samia ameridhia ombi hilo lililotolewa na Prof. Lumbu aliyefika Ikulu jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuonana na Rais na kujadili mambo mbalimbali yanayohusu masuala ya Haki za Binadamu na Watu huku akiambatana na wadau wa asasi za kiraia za kutetea haki za binadamu za hapa nchini leo Tarehe 30/01/2023.

Awali kabla ya kuwasilisha ombi hilo, Prof. Lumbu alianza kwa kupongeza hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita ikiwa ni pamoja na uhuru wa kujieleza ambapo makundi mbalimbali yameonekana kupewa nafasi ya kujieleza yakiwemo makundi ya wanasiasa, Pia aliongelea suala la uhuru wa vyombo vya Habari ambao unaonekana kuimarika na jitihada mbalimbali zilizofanyika katika kukuza matumizi ya Lugha ya Kiswahili.

Baada ya pongezi hizo Prof. Lumbu aliwasilisha ombi hilo rasmi kwa Mhe. Rais huku akimuomba pia kuwa mgeni rasmi katika mkutano huo ambapo Mhe. Rais aliahidi kutoa jibu baadae juu ya hilo.

Akiongelea suala la maendeleo ya haki za binadamu, Rais Samia alisema anaamini kuwa matatizo ya ndani yanaweza kumalizwa na sisi wenyewe na sio mtu wa nje na ndio maana alifikia hatua ya kukutana na vyama vya upinzani na kuangalia changamoto ni nini na baada ya majadiliano ikafikia hatua ya maridhiano yaliyopelekea pande zote kuwa kauli moja na hivyo kuondoa migongano.

MwishoRais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu Mhe. Prof. Remy Ngoy Lumbu.

Previous articleEFTA KUWEZESHA WAKULIMA ZAIDI YA 200 KUPATA MIKOPO YA MATREKTA BILA DHAMANA
Next articleDIWANI MARIAM LULIDA WAFANYA ZIARA SGR MIAKA 46 YA CCM
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here