Home BUSINESS ACT WAZALENDO KUZINDUA MIKUTANO YA HADHARA JIJINI DAR ES SALAAM

ACT WAZALENDO KUZINDUA MIKUTANO YA HADHARA JIJINI DAR ES SALAAM

(PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo, DSM

Chama cha ACT Wazalendo Kimetangaza rasmi ratiba ya kuanza kwa mikutano ya hadhara itakayofanyika katika awamu mbalimbali nchi nzima.

Akitoa tangazo hilo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Januari 22,2023 katika Ofisi za Chama hicho Jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Chama hicho Ado Shaibu amesema kuwa mikutano hiyo itaanzia Jijini Dar es Salaam na kwamba huo ni uamuzi wa kamati Kuu ya Chama hicho iliyoketi Januari 21 mwaka huu.

Akizungumzia ratiba ya mikutano hiyo, katibu Mkuu huyo amesema kuwa  awamu ya kwanza, Program ya Kitaifa ya Mikutano ya hadhara inajumuisha mikoa ya Dar es Salaam Februari 19,2023 Unguja, Februari 26,2023, Pemba Machi,2023, Tanga Machi 08,2023 na Pwani Machi 09,2023. 

Mikoa mingine ni pamoja na Lindi Machi 10, 2023, Mtwara Machi 11,2023. Mkoa wa Kichama Selous Machi 12, 2023, Tabora Machi 14,2023 na Kigoma Machi 16-18, 2023.

Awamu ya pili ya mikutano ya hadhara itatangazwa baadaye.

“Agenda kuu zitakazotawala na kuongoza mikutano ya ACT wazalendo ni hali ya maisha ya wananchi na mageuzi ya mifumo ya kidemokrasia nchini”

“Kamati Kuu imeelekeza kuwa mbali na ajenda nyinginezo muhimu, Mikutano ya Hadhara ya Chama pia itumike kutambulisha Ahadi za Chama chetu (ACT BRAND PROMISE)
kwa Watanzania na Wazanzibari ambapo Chama kitachambua changamoto mbalimbali zinazoikabili nchi, namna watawala wameshindwa kuzitatua na kuonyesha sera mbadala za ACT Wazalendo kutatua changamoto hizo.” amesema Ado.

Aidha Kamati Kuu imeiomba Serikali ya Jamhuriya Muungano wa Tanzania na Zanzibar kuweka wazi kalenda ya utekelezaji wa mapendekezo ya Ripoti za Vikosi Kazi vya Demokrasia pamoa na  kalenda ya mchakato wa uundwaji wa Tume Huru ya Uchaguzi.

“Tunaiomba Serikali za Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Zanzibar, ziweke bayana kalenda na mchakato wa uundwaji wa Tume Huru ya Uchaguzi.” amesema Ado Shaibu,  na kuongeza kuwa

“Kamati Kuu ya ACT Wazalendo inataka maelezo ya kina kuhusu uundwaji wa Kamati ya Uteuzi ya Wajumbe wa Tume za Uchaguzi NEC na ZEC (Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Mkurugenzi na Wajumbe) na upatikanaji wa Wajumbe hao” ameongeza.

Pia Kamati Kuu ya ACT Wazalendo imeiomba Serikali kuweka wazi ni lini mchakato wa Katiba Mpya utaanza, hasa hatua muhimu za kupitiwa upya kwa sheria ya Mabadiliko ya Katiba (Constitutional Review Act) na Sheria ya kura ya maoni.

Previous articleTANI 13 ZA SIGARA BANDIA ZATEKETEZWA GEITA.
Next articleDKT. BITEKO AWATAKA WATUMISHI WA STAMICO KUENDELEA KUNG’ARISHA SHIRIKA LA MADINI.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here